skip to main content
The problem of waste
Waste

Changamoto la taka

Kote duniani, vitongoji duni vinakabiliana na changamoto ya kiafya na kimazingira kutokana na kukosekana kwa njia mwafaka ya kushughulikia taka. Katika jiji la Kisumu, wenyeji wanatumia taka kutengeneza vifaa mbalimbali.

Simulia Hadithi, Shiriki Suluhu

Jinsi changamoto inavyozungumziwa,  inavyojadiliwa, na sauti zinazosikika katika mjadala huu zinaweza athiri matokeo baadaye. Mradi wetu unafundisha wanahabari kuandika kwa kina jinsi taka inavyoathiri mazingira na afya ya Kisumu. Vijana ambao wanaishi katika vitongoji vilivyoathiriwa zaidi wanafanya kazi nao, na wanajifunza jinsi ya kusimulia hadithi zao na kushiriki maoni na suluhisho za jamii zao.

Mnamo Machi 2021, wanawake kutoka vitongoji duni vinne vya Kisumu walikusanyika kujadili suluhisho zao za kudhibiti taka katika vitongoji vyao. Filamu hii inasimulia hadithi ya Wilkeister, mfanyibiashara mwenye umri wa miaka 65 kutoka Manyatta A na mwanachama wa Kikundi cha Wanawake cha Flamingo Jikaze. Kikundi hiki huleta akina mama pamoja 'ili waweze kuboresha maisha yao'. Wilkeister anaunda mifuko, mikeka na bidhaa zingine nzuri kutoka kwa taka, na kusuka mifuko ya plastiki na sindano kutoka kwa miavuli iliyovunjika. Kwa akina mama hawa, imekuwa chanzo muhimu cha mapato. Pamoja, wanashirikiana na wanawake kutoka makaazi mengine, wakiwaeleza hadithi zao wakitarajia kupanua masoko yao na kuboresha vitongoji hivi vyote, ambapo ukosefu wa ajira uko juu.